Wizara ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inalaani vikali tukio la kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4, ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii.
Wizara hiyo imesikitishwa na mazingira ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi. Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi.
Inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
Wizara ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Hii Wizara ambayo haikutajwa - ni ya uchukuzi? ulinzi? afya? madini? TAMISEMI? mambo ya ndani?
ReplyDelete