Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo yanayohusisha walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.
Programu hiyo inayotoa ushirikiano mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
Mpango huo ambao kwa ujumla wake , awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha kwa kutumia Tehama.
Mradi huo unaojulikana kama UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam.
Walioketi kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...