Mshauri Mganga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hosipitali ya Shree Hindu Mandal, ambaye pia ni Katibu wa kitengo cha Watafiti wa ugonjwa wa kisukari Afrika Mashariki (EADSG) Dkt. Kaushik Ramaiya alisema umuhimu wa mbinu ya Taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa kisukari ni nyenzo muhimu kwa Taifa hili. Kushoto ni Pro. Ayoub Magimba - Kutoka Wizara ya Afya Tanzania,Dkt. Steven Shongwe, WHO-AFRO na kulia ni Dkt. Mr. Anders Dejgaard: Mkurenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kisukari Duniani (World Diabetes Foundation)
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kisukari Duniani (Wolrd Diabetes Foundation) Dkt Anders Dejgaard akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa wadau wa kisukari uliopangwa kuanza tarehe 17 na 18 katika ukumbi wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere Convention Centre.
Mkutano huo utahusisha Viongozi wa Mfuko wa kusaidia wagonjwa wa Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani watakaokutana kujadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa ishio na Kisukari.
Tarehe 17 na 18 March 2016 Dar es Salaam, TANZANIA
MKUTANO huo maalum wa siku mbili wa wadau wa kisukari duniani ambao utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.
Mshauri Mganga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hosipitali ya Shree Hindu Mandal, ambaye pia ni Katibu wa kitengo cha Watafiti wa ugonjwa wa kisukari Afrika Mashariki (EADSG) Dkt. Kaushik Ramaiya alisema umuhimu wa mbinu ya Taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa kisukari ni nyenzo muhimu kwa Taifa hili.
Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Mkutano huo Dkt Kaushik alisema "Linapokuja suala la kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kisukari Mkutano kama huo unachukua nafasi kubwa kwa wagonjwa waishio na Kisukari,”
"Kwa kuimarisha kile ambacho tumejifunza, na kubadilishana mambo muhimu miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, tutakuwa na uwezo wa kuwezesha yatokanayo baada ya Kongamano la Kisayansi na utafiti katika kufikia malengo, Mpango wa WHO Global Action kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, unahitajika."
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...