Zaidi ya wananchi elfu moja kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamewekwa kizuizini kwa muda wilayani Babati baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. https://youtu.be/L0pqIWZUrCA  

Kamati ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii yaahidi kushirikiana na serikali kupitia TAMISEMI kuhakikisha inaimarisha bajeti ya wizara kwa kuwa sekta ya afya inamgusa kila mtanzania. https://youtu.be/UhfFys0X7UI  

Shirika la viwango nchini TBS lafunga biashara ya maduka manne ya kuuza vifaa vya umeme wa jua Solar katika eneo la Kariakoo baada ya kubainika vifaa hivyo kukosa ubora unaokubalika. https://youtu.be/wO6gSULsMIU  

Waziri mkuu Khasim Majaliwa afanya ziara ya kushitukiza katika soko la Ferry kuiagiza bodi ya soko hilo kukutana na makampuni mbalimbali yanayouza gesi ili kupata gesi ya bei nafuu ili kuwapunguzia gharama wakaangaji wa samaki sokoni hapo.https://youtu.be/tW-UFkS3K88  

Waziri mkuu Khasim Majaliwa afanya ziara ya kushitukiza soko la Ferry na kuiagiza bodi ya soko hilo kutafuta unafuu wa bei ya gesi. http://simu.tv/YMM4Guh  

Mkurugenzi mku mpya wa TBC Dr. Ayoub Rioba akaribishwa ofisini na mtangulizi wake Clement Mshana. https://youtu.be/drZ6QJMzpqQ   

Wanawake huko wilayani Handeni mkoani Tanga walalamikia tabia ya baadhi ya wanaume kuwanyanganya fedha wanazopewa kwa ajili ya kujikimu kupitia mfuko wa TASAF. https://youtu.be/H7HaKoCBB7k

Mvua kubwa ya mawe iliyoambana na upepo mkali imeezua nyumba zipatazo 9 na kuharibu mashamba huko wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.https://youtu.be/5PAPWW_sisI  

Waziri Wiliam Lukuvi aliagiza Shirika la Nyumba la Taifa NHC, kutoanzisha mradi mipya mikubwa hadi pale miradi iliyopo itakapo malizika. https://youtu.be/huyG6dijTvcv
  
Harakati za maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar Dr.Shein zendelea katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar. https://youtu.be/b-pJy2jd6oI

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimezindua rasmi kozi ya diploma ya lugha ya kichina itakayoanza kutolewa mwakani. https://youtu.be/8dfv3bGev7Y  

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amefanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu za bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza. https://youtu.be/F9nbSfmHw7Q  

Rais Magufuli amemtumia salamu za pole mkuu wa mkoa wa Njombe kufuatia kifo cha ghafla cha mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba. https://youtu.be/0a7-zE-nKdU


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...