Mhe. Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumzia uzefu wa Tanzania katika kukabiliana na tatizo la ukeketaji akiwa na wazungumzaji wengine katika Meza Kuu, kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Burkina Faso Bi. Sika Bella Kabore, Bw. Benoit Kalasi (UNFPA), Bi.Emma Bonino Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Italia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mhe. Peter Serukamba akifuatilia majadiliano kuhusu tatizo la ukeketaji na adhari zake wa afya na maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke.
Wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi nao wakifuatilia majadiliano yaliyovutia washiriki wengi kuhusu madhara yatokanayo na ukeketaji na namna gani jamii inatakiwa kushirikiana kutokoza tatizo hilo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano na majadiliano kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukeketaji na uhusiano wake na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huu uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Burkina Faso, Italy, Iran, UNFPA na UNCEF.
Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb) amesisitiza kuwa ni kwa ushirikiano baina ya Serikali na jamii ndipo tatizo la ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake litakapoweza kutokomezwa.
Akaongeza kwamba, serikali inaweza kutunga sheria nyingi za kukabiliana na tatizo hilo lakini kama jamii yenyewe kuanzia ngazi ya familia isipotoa ushuriano wa dhani itachukua muda mrefu kwa tatizo hilo kutokomezwa. Alikuwa akizungumza wakati wa majadiliano ya mkutano wa kuhusu utokomezwaji vitendo vya ukeketaji kama sehemu muhimu ya utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030.
Waziri Ummy Mwalimu alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika mkutano huo uliowahusisha Mke wa Rais wa Burkina Faso, Bibi. Sika Bella Kabore, Mawaziri na Asasi za Kiraia na uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za kudumu za Tanzania, Italy, Iran, Burkina Faso,UNFPA na UNICEF, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake.
Na kwa sababu hiyo, Waziri Ummy Mwalimu, amerejea kutoa wito kwa watanzania wote kwa katika ujumla wao wakiwamo wazee wa kimila, viongozi wa dini na vijana wakiume kutoa ushirikiano kwa serikali na wadau wengine ili hatimaye tatizo hilo ambalo linaelezwa kuwa siyo tu lina madhara makubwa kiafya na kisaikolojia lakini pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Tunatakiwa kufanya kazi kwa pamoja na katika umoja wetu, serikali peke yake haitaweza kulimaliza tatizo hili, ambalo imefikia mahali sasa wazazi kwa kuongopa mkono wa sharia wanaamua kuwafanyia ukeketeji watoto wa kike katika umri mdogo sana” Akaeleza Waziri.Akasema , Tanzania imebaini uelimishwaji na majadiliano yanayohusisha familia na vijana wakiume ni muhumu katika kuchangiza juhudi za serikali katika kukabili ukeketaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...