Mhadhiri wa Idara ya Sayansi
ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John
akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali katika
utoaji wa ripoti ya CEMOT iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waliokuwa waangalizi katika uchaguzi 2015 wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Mradi-CEMOT Bwa.Bernard Kindoli akizungumza na waliokuwa waangalizi wa
uchaguzi majimbo mbalimbali katika utoaji wa ripoti iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CEMOT,Bi.Harusi Miraji akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali wakati utoaji ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waangalizi wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
RIPOTI ya Muungano wa Asasi za Kitanzania zinazoangalia uchaguzi nchini kwa Kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CEMOT) imesema kuwa, kuweza kupata uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake kwa upande wa wanawake itachukua miaka 150 kutokana na ushiriki wao kuwa mdogo katika nafasi za kugombea.
Akizungumza na waangalizi wa uchaguzi wa mradi wa CEMOT, kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John amesema kuwa ushiriki wanawake ni mdogo katika nafasi mbalimbali za kugombea na kufanya uwakilishi wa 50 kwa 50 kuchukua muda mrefu.
Amesema kuwa wanawake waliogombea katika kiti cha urais kwa kuchaguliwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa saba lakini hawakuweza kuingia katika nafasi ya kwanza ya kupeperusha bendera.
Dkt.John amesema kuwa wanawake waliogombea katika nafasi ya ubunge kwa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi wa mwaka 2015 walikuwa 238 walioweza kuchaguliwa katika nafasi hiyo ni wabunge 24 tu .
Amesema kuwa ushiriki wa uchaguzi kwa wanawake ongezeko kwa mwaka 2015 ilikuwa asilimia 2 ambayo ni kiwango kidogo katika kuweza kufikia asilimia 50 kwa 50.
Ripoti hiyo pia imesema kuwa wanawake katika nafasi ya urais ni mwanamke mmoja tu ndio aliweza kupeperusha bendera ya chama chake hali ambayo katika nafasi hiyo ni ndogo ya kufikia uwiano huo.
Wazo la 50-50 ni baya kabisa kwani litaendelea kuwakandamiza wanawake na kuwapendelea wanaume pale ambapo asilimia ya wataalam wanawake ni kubwa kuliko asilimia ya wanaume.
ReplyDeleteEng. UAE.