BENKI ya Exim Tanzania imeshiriki kikamilifu kwenye mbio za tisa za Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa kupitia mbio hizo katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria hapa nchini.

Mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Karatu chini ya ushiriki wa Waziri wa Maliasiri na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa mgeni rasmi zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria sambamba na kusaidia elimu ya awali kwa jamii wa Wamasai waishio jirani na kivutio hicho.

Mbali na kushiriki katika udhamini wa mbio hizo baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walijumuika na washiriki wengine katika mbio za kilometa 5 zilizohusisha kundi la washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporate challenge category). Watoto pia walipewa fursa ya kukimbia mbio fupi za kilometa 2.5, wakati shindano refu lilikua la kilometa 21 tokea Ngorongoro hadi Karatu.

“Ni wazi kwamba taasisi za kifedha tukiwemo Benki ya Exim ustawi wetu unategemea sana uwepo wa jamii yenye afya na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kushiriki mbio hizi kwa maana ya kuhamasisha michezo lakini pia kuunga mkono malengo yake yaani kuikabili malaria na kusaidia elimu,’’ alisema mwakilishi wa benki hiyo Bw. Emmanuel Mwamkinga, meneja wa benki ya Exim tawi la Karatu.

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kushiriki katika kusaidia michezo na matukio mbalimbali hasa yale yenye kuleta tija kwa jamii hususani kwenye sekta ya afya, elimu na mazingira.

Katika mbio hizo zilizoanzia katika lango la kuingilia na kutokea Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia kwenye uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu ilishuhudiwa mwanaridha Ismail Juma akivunja rekodi ya mbio hizo kwa kutumia saa 1:02:48 na kuipiga kikumbo ile ya awali ya saa 1:03:00 iliyowekwa miaka ya nyuma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii prof Jumanne Maghembe akimpongeza meneja wa benki ya Exim tawi la Karatu Emanuel Aaron kwa kupata tuzo ya ushiriki wa mashindano ya Ngorongoro marathon yaliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha.
 Meneja wa Benki ya Exim tawi la Karatu Emanuel Aaron akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya ZARA Zainab Ansell,kwa  ajili ya ushiriki wa mashindano ya Ngorongoro marathon  yaliyo fanyika wilayani Karatu mkoani Arusha.

  Waziri wa maliasili na utalii prof Jumanne Maghembe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim mara baada ya kutembelea banda siku ya mashindano ya Ngorongoro marathon yaliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha..
Afisa masoko wa Exim benki wa kwanza (kushoto),meneja mauzo Zaitun Mussa (katikati) na Meneja wa tawi la Karatu Emanuel Aaron wakiwa na tuzo yao waliyo ipokea siku ya Ngorongoro Marathon yaliyofanyika wilayani Karatu,Arusha
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...