Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) Bw. Jerry Sabi akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa
Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa TAHLISO Bw. Stanslaus Kadugalize.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu
(TAHLISO) kutoka Chuo Kikuu cha Bugando Bw. Elia Kandonga akiongea katika mkutano kati ya
TAHLISO na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na kufanyika mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wahitimu bora wa vyuo vikuu mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandishi Stella Manyanya katika hafla iliyoandaliwa na
Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) ili kuwapongeza na kufanyika
mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) kutoka vyuo mbalimbali nchini katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) waliokutana katika Chuo Kikuu cha Mt. John mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wamekutana mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ili kubadilishana mawazo na kukubaliana kuendeleza ushirikiano ili kutatua kero za wanafunzi.
Katika mkutano huo, uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAHLISO kutoka taasisi za elimu ya juu nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw. Peter Kadugalize walikutana kwa siku nzima na viongozi wa HESLB walioongozwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi na kujadiliana njia bora za kutatua kero za wanafunzi.
Linaloonekana nyuma ni ndo majengo JPM anapiga nayo kelele. Tumsaidie rais wetu. Hapo hata wakitangaza siku ya kujitolea wanachuo wenyewe wanaweza kupanga rangi. Ankal tafadhali wafikishie ujumbe na uwashauri. Sio kila kitu kinahitaji wakandarasi.
ReplyDelete