NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.


Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara.

Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong'oto.
Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu.
Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...