Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Je, kuna wakati utafika misingi ambayo taifa hili lilijengwa kwahiyo, itapitwa na wakati? Je, tuachane na mbio za Mwenge kwa sababu za gharama kuwa kubwa - wengine wanasema mwenge ni Jipu na Rais Magufuli alitumbue? Au Mbio za Mwenge zina umuhimu na ni sehemu ya msingi ambao taifa hili lilianzishwa na ni kumbukumbu ya mapambano ya kumletea mabadiliko na maaendeleo Mtanzania? Yote haya nitayatolea ufafanuzi kwenye Penyenye Fupi Fupi.


Falsafa ya Mwalimu Julis Kambarage Nyerere kuhusu mwenge wa Uhuru ilikuwa ni: “Sisi Watanganyika, tunataka  kuuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”.

Je, Falsafa ya Kuanzishwa kwa Mbio za Mwenge wakati wa Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/1961 imepitwa na wakati??? Ikumbukwe kwamba falsafa hii ni sehemu ya misingi ya Taifa letu..tangu ilipoanzishwa na waasisi wetu. Mataifa yaliyoendelea yameendelea kuenzi misingi iliyojenga Mataifa hayo kwa gharama zozote zile. Tutakubaliana sote kuwa Watanzania bado tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye ujinga, maradhi, na umaskini. Tunahitaji kujikwamua kutoka kwenye dhuruma na chuki ambazo, ukizingatia dhana ya mazingira na wakati, zimekuwa ni tofauti zaidi ukilinganisha na wakati wa Uhuru. Japokuwa wakati wa Uhuru kulikuwa na dhuruma, ufisadi, chuki nakadharika, bado hata sasa hivi tuna ufisadi, dhuruma na chuki tena zilizoenda mbali sana. Katika dhama hizi za Magufuli, zilizotofauti kabisa na nyakati za Kikwete, Mkapa, Mwinyi na zile za wakati wa Baba wa Taifa. Tumejionea uozo wa hali ya juu kuliko ambavyo tumewahi kushuhudia. Neno hili siyo geni tena kwetu – “Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi”.  Mwenge wa Uhuru unapaswa kutukumbusha kila mara kuwa vita dhidi ya ubadhirifu, chuki, na dharau bado inaendelea. Tena falsafa ya Mwalimu ilikuwa inataka huu Mwenge umulike hadi nje ya mipaka yetu. Hii inanipeleka kwenye penyenye yangu inayofuata – Kuingiliwa kwa Uhuru wa Taifa letu na Mataifa ya Magharibi.

Tutakumbuka kuwa hivi karibuni sakata la MCC 2 lilishika kurasa nyingi sana. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar na kuhusiana na ile sharia ya makosa ya Kimtandao. Taasisi ya MCC ni kibaraka wa umagharibi, pia ina kila lengo la kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu. Maitaifa ya Magharibi kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika limekuwa ni jambo la kawaida sana. Tumekuwa ni nchi ya amani isiyokiuka haki za binadamu, sasa kuiingiliwa kwenye mambo ya ndani ya nchi ni jambo linakiuka hadhi yetu ya kuwa Sovereign State. Mwenge wa Uhuru unatukumbusha maneno ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa “… tunataka kuuwasha Mwenge na kuuweka juu yam lima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu...” Je msingi huu wa kuanzishwa kwa Taifa letu umepitwa na wakati, hasha.. msingi huu bado uko na unaendelea. Na kama taifa lazima tusimame kidete. Mwenge huu inabidi tuumulike ili sisi kama Watanzania tujikumbushe, na hayo mataifa ya nje yaliyo karibu nasi na yaliyo Magharibi au Mashariki. Pia ninaungana na kauli ya Mh. Rais Dk. John Joseph Magufuli kuwa ni bora kuishi kwa kula mihogo kuliko kula mkate ya masimango.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...