Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bi. Zena Kongoi ameupongeza mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera kwa kuendelea kuwa mfano wa mgodi pekee hapa nchini unaomilikiwa na serikali kwa 100% na kuzalisha dhahabu chini ya Wataalam wa Kitanzania pekee.

Pongezi hizo zilitolewa wakati wa ziara yake hapa mgodini mwishoni mwa juma iliyolenga kuzungumza na Wafanyakazi na kuelezea dhamira kuu ya STAMICO ya kuhakikisha mgodi huu unasonga mbele pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi hususani suala la ufinyu wa mtaji na kuahidi kuwa Shirika limepanga kwa mwaka huu wa 2016 fursa zote zinazohusu madini zinaunufaisha mgodi wa STAMIGOLD.
“ Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya pamoja na uwepo wa changamoto nyingi na hasa ya ufinyu wa mtaji lakini bado mnaendelea kutumia ubunifu na uzalendo wenu kuendesha mgodi na kuzalisha dhahabu hivyo kwa niaba ya STAMICO tunawapongeza sana na tunatambua kazi yenu nzuri mnayofanya ukizingatia kuwa moja ya malengo ya serikali ya sasa ni kuhakikisha uchumi wa madini unarudi kwa Watanzania na kwa kupitia mgodi huu mmeweza kuonyesha kuwa hilo linawezekana” Alisema Bi. Kongoi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...