Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe) akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania Bi. Sherry Mavura (wa kwanza kulia) msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo Sabuni, Unga, Mchele, Mafuta, miswaki, dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha kituo hicho.
"Leo mchana Aprili 10, 2016 nimesherekea siku yangu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 10 ya Uandishi wa Habari na watoto Yatima wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar kwa kula nao chakula, kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapa msaada wa vitu mbali mbali. Nawashukuru wale wote walioungana na mimi. Mungu awabariki sana" alisema Kajuna.
 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akiwagawia juisi watoto yatima wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye  kituo cha kulelea  watoto yatima cha kituo cha SOS Children's Village Tanzania.
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna pamoja na mwenyekiti wa Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw. Joachimu Mushi wakiwa kwenye pozi na watoto. Mwenyekiti wa TBN ni mmoja ya wageni waalikwa waliosindikiza.
Cathbert Angelo Kajuna kiimbiwa wimbo na familia yake pamoja na baadhi ya watoto yatima wakati wa ukataji keki aliyokula na watoto hao katika kituo cha ha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...