Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya
Nigeria Super Eagles Nwankwo Kanu leo ametembelea Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete katika Hopsitali ya Taifa Muhimbili (NH) kwa lengo la kuwajulia
hali wagonjwa wa moyo ambao wamelazwa katikaTaasisi hiyo, pia kubadilishana
uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi hiyo.
Akizungumza baada ya kuwasili
katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa
kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuwapa pole.
Katika mazungumzo yake pamoja na mambo
mengine Kanu ameonyesha nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi ya Moyo ili
kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo
na kwamba watazungumzia suala hilo.
Pia, ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa
Watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara
kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona.
Kwaupande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa
watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Godwin Godfrey amesema tangu
Julai mwakaja na mpaka sasa taaissi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka
nje ya nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu alifanyiwa upasuaji wa moyo
mwaka 1996 na ndipo aliamua
kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa The Kanu Heart Foundation.
Kanu amechezea timu ya Taifa ya Nigeria
yaSuper Eagles, Arsenal, Inter Milan, West Bromwich Albion, Portsmouth na AFC
Ajax. Amenyakua tuzo nyingi kutokana na umairi wake soka.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super
Eagles, Arsenal, Inter Milan, West Bromwich Albion, Portsmouth na AFC
Ajax,Nwankwo Kanu akilakiwa na Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo, Dk Peter Kisenge, katika taasisi hiyo
akimkaribishaNwankwo Kanu leo. katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea
wagonjwa wa moyo leo.
Fatuma Shaban akipokea
zawadi kutoka kwa Nwankwo Kanu kwa niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye
amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.
Mgonjwa Mariam Omary akifurahia jambo baada ya mchezaji huyo kumjulia hali leo
kwenye taasisi hiyo.
Mchezaji huyo akiwa katika
chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) leo.
Kanu akipata maelezo kuhusu Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hopsitali ya Taifa Muhimbili
Mchezaji huyo akieleza historia fupi baada ya kubainika kuwa na tatizo
la moyo miaka ya tisini na kutokana na tatizo hilo aliamua kuanzisha mfuko wa
kusaidia watu wenye matatizo ya moyo. Mfuko huo unajulikakanaKanu Heart Foundation.
Picha zote na John Stephen, Ofisa Uhusiano
wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...