Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kufanya
tafiti na kuangalia fursa zitakazoiwezesha kupata mapato kutokana na kazi
inazozifanya.
Amesema iwapo
Mamlaka hiyo itafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu itaongeza idadi ya watu
inaowahudumia kwa mwaka nchini na hivyo kusaidia wadau mbalimbali wa sekta za
Kilimo, Ujenzi, Afya, Uvuvi kufanya kazi kwa faida.
Prof. Mbarawa
amekagua vitengo cha takwimu za hali ya hewa, hali ya hewa ya kilimo na Utabiri
na kusisitiza kuwa ni wakati wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa teknolojia ya
kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati mmoja.
“Hakikisheni
taarifa zenu zinawafikia watu wengi hususan wale wanaozihitaji taarifa hizi kwa
kutekeleza shughuli zao kiuchumi”. Amesema Prof. Mbarawa.
Naye
Mkurungenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa
Mamlaka hiyo inafanya utabiri kwa
usahihi wa asilimia 80 na ni miongoni mwa Mamlaka inayofanya vizuri katika
huduma za utabiri barani Afrika.
“Taarifa zetu
ni sahihi na kila baada ya dakika 15 tunatoa taarifa zinazoonyesha hali ya hewa
nchini”. Amesema Dkt. Kijazi.
Dkt. Kijazi
amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uelewa wa watumiaji wa hali ya hewa
hapa nchini ili kuwezesha wadau wa hali ya hewa kunufaika kikamilifu na utabiri
unaotolewa na Mamlaka hiyo.
Imetolewa na
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma ramani ya
utabiri wa hali ya hewa katika chumba maalum cha kusoma ramani wakati wa kukagua ofisi za Mamlaka ya hali ya hewa nchini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Watatu kushoto) akifafanua
jambo kwa wafanyakazi wa mamlaka ya hali
ya hewa nchini (Hawapo pichani) huku Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agness Kijazi
( Watatu kulia) akifuatilia kwa makini.
Mtaalamu
wa maswala ya hali ya hewa nchini Didasian Kankesha akifuatilia utabiri kabla
ya uhakiki na kuutangaza kwa wadau.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi
wa TMA kuhusu namna ya kufanya kazi kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ili
kuhudumia wadau wengi kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...