Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.
Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika Serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...