Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Safi sana wabunge. Nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe. Hizi ni ela nyingi sana. Kumbe mambo yanawezekana. Nimesoma taarifa kuwa ikiwa spirit hii itaendelea Tanzania inaweza kuipiku Kenya kiuchumi. Tusonge mbele kwa pamoja.
ReplyDeleteAmen mdau
DeleteZaidi, tunaweza kuachana na mapesa ya Marekani ya MCC!
ReplyDeleteUjumbe uko wazi mwenye asikio na asikie tutumie rasilimali zilizopo kujikwamua kutoka katika maisha duni ya kuwa na mapato yasiyotosha kwa sababu ya matumizi mabaya, kwa nini baada ya miaka yote ya uhuru tukose maji,tuwekeze kwenye miundo mbinu ya maji, wanafunzi wae na madawati, kila mtanzania awe na nyumba bora ili hata kulala kusiwe shida umeme uwepo kwa wote n.k. Kila mtu akifanya wajibu wake inawezekana
ReplyDelete