Bi.Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo, lakini matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye hospitali wanakotoka.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH.

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, MNH, na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu), waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.
Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu

“Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi wa habari leo Aprili 25, 2016.

Hofu ya wagonjwa.
Awali baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...