Kuelekea siku ya Malaria Duniani ambayo kitaifa huadhimshwa tarehe 25
Aprili, Shirika la Afya na Elimu
ya Tiba (TAHMEF) limetoa huduma ya upimaji wa Afya tarehe 23 Aprili
katika msikiti wa Masjid Al Ghadir, uliopo Kigogo, Jijini Dar es salaam.
Huduma hiyo ilihusisha upimaji wa Malaria, kisukari, shinikizo la damu na upungufu wa damu, ambapo Matibabu ya
Dawa na ushauri ulitolewa kwa wananchi waliobainika kuwa maradhi hayo, chini ya uangalizi wa madaktari
wazoefu.
Jumla ya wananchi 352 walipata huduma hii, wanawake wakiwa 150 na wanaume 202 kati ya idadi hiyo.
Mkazi wa kigogo akipata Huduma ya upimaji Wa Afya katika zoezi lililoendeshwa na TAHMEF.
Muanzilishi wa TAHMEF, Bi. Juliana Busasi (aliembeba mtoto) akisaidia katika kufanikisha upimaji wa malaria kwa mtoto ambaye ni mkazi Wa kigogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...