Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TIMU ya Mpira wa Pete ya Wanawake wa Idara ya Uhamiaji imebuka mshindi wa tatu katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kaimu Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli amesema kuwa washindi wa tatu ni mwanzo wa kujipanga mashindano mengine katika kuibuka kuwa washindi wa kwanza.
Amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa wanamichezo katika wa idara hiyo kuendeleza vpaji wa vya watumishi katika sekta ya michezo.
Nahodha wa Timu hiyo, Juliana Mwakalemela amesema kuwa katika mashindano hayo idara ya uhamiaji ndio pekee walioshiriki mashindano hayo.
Juliana amesema kuwa kikombe cha mshindi waa tatu ni nyota njema katika kujiandaa mashindano mengine na kuweza kuibuka washindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...