Wachezaji wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club, Grace
Mwasote (kushoto mwenye mpira) akizuiwa na Johari William wakati wa
mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini mwishoni mwa wiki.
Timu hiyo inajiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika mjini
Dodoma.
Grace Mwasote akiwa na mpira akiangalia jinsi ya kuwatoka
wachezaji wenzake wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club. Wengine
pichani ni Johari William (kushoto) na Maimuna Ayelo.
Matalena Mhagama mfungaji mkongwe pia wa timu ya Taifa ya netiboli(kushoto), akizuiwa
na Sharifa Mustafa (kulia) huku Mary Kajigili (kushoto nyuma),akiangalia.
Maimuna Ayelo (kushoto) akidaka mpira huku Subira Jumanne
akijiandaa kumzuia katika mazoezi ya timu ya netiboli ya Uchukuzi yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Bandari Kurasini, wakijiandaa na mashindano ya Mei Mosi.Imetolewa na
kitengo cha Sheria na Mahusiano - TAA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...