Bodi ya Utalii Tanzania imekutana na wadau wa Utalii wa Tanzania kwa lengo la kujadili namna watakavyoweza kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania.

Mkutano huo uliohudhuliwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya utalii vya Tanzania; Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT), Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Chama cha Waendesha Safari za Anga Tanzania (TAOA) na Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TASOTA)

Aidha, katika mkutano huo wadau waliweza kutambulishwa tovuti maalumu (Tourism Destination Portal), ulioandaliwa na TTB kwa ajili ya kuboresha utangazaji wa utalii kupitia TEHAMA. Tovuti hiyo inapatikana kwenye http://www.tanzaniatourism.com/en.

Mkutano huo ulifanyika tarehe 20/04/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii, Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi (kulia) akiongea na wadau wa Utalii katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Utalii Tanzania, Bw. Richard Rugimbana (katikati) akitoa maelezo katika moja ya mada zilizoongelewa kwenye mkutano huo. Aliyekaa upande wa Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania, Bi Latifah Sykes pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi.
Wengine ni Baadhi ya wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya utalii Tanzania waliyohudhulia ni Bw. Laurence Paul (Katikati) ambaye ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Waendesha Safari za Anga Tanzania, kulia kwake ni Bw.Moses Ngereza wa Shirikisho la Utalii Tanzania na Bi E. Fernandes wa TASOTA
Washiriki wote wa mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tunahitaji kuutangaza utalii na kuboresha huduma zinazotolewa, tukilinganisha na nchi nyingi vivutio tunavyo vingi kazi kwetu kuutangaza utalii na kuwa mwenyeji wa matukio ya kimataifa ikiwemo mikutano mikubwa itakayowezesha hoteli kubwa zilizopo kuchangia uchumi.

    ReplyDelete
  2. Watu wetu lugha tatizo! Wataitangazaje huko nje? Kwa Kiswahili?

    ReplyDelete
  3. Hawa wawakilishi wao kiingereza wanajua bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...