Mwimbaji nyota wa Mashujaa Band Chaz Baba, leo usiku atakwea
jukwaa la Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden Kinondoni katika
onyesho maalum la “Usiku wa Kismet”.
Katika onyesho hilo, Chaz Baba ataimba wimbo wa Isha Mashauzi
“Nani Kama Mama” pamoja na vionjo vyake kadhaa vya nyimbo zake
za dansi.
Usiku wa Kismet umeandaliwa maalum kwaajili ya watu kujiachia na
wapenzi wao ambapo pia CD za wimbo wa “Kismet” zitatolewa kama
zawadi ukumbini.
“Kismet” ni wimbo mpya wa Mashauzi Classic ulioimbwa na Isha
Mashauzi ambao umejaa maishairi matamu ya mapenzi.
Akiongea na mtandao huu, Isha Mashauzi ambaye ndiye bosi wa Mashauzi
Classic, alisema mashabiki watakaoweza kuimba kwa ufasaha japo
mstari mmoja wa wimbo “Kismet” watazawadiwa zawadi ya fulana za
Mashauzi Classic.
Awali “Usiku wa Kismet” ulikuwa ufanyike Alhamisi iliyopita lakini
ukaahirishwa kutokana na mvua mkubwa iliyonyesha katika muda
mwingi wa onyesho hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...