Mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM) Mkoa wa Kigoma peter Msanjilla akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake(hayupo pichani) baada ya kikao cha kamati ya  utekelezaji umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kigoma

Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma. 

UMOJA wa vijana wa chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kigoma wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri anayofanya ya kuwatumikia wananchi tangu alipoingia madarakani. 

Mwenyekiti wa umoja huo wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Peter Msanjilla, alimwambia mwandishi wa blog hii ofisini kuwa kamati ya utekelezaji ya vijana Mkoa wametoa pongezi hizo katika kikao kilichofanyika leo (jana) kwenye ofisi za CCM mkoa. 

Alisema kuwa wameamua kumpongeza Rais kwa sababu ya kasi yake anayofanya ya kudhibiti uchumi na kutaka nchi ijiendeshe kwa kutumia fedha za ndani. Msanjilla alisema kuwa pia katika kikao hicho wamemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais kwa kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo katika Mkoa akishirikiana na mamlaka ya mapato nchini(TRA). 

"Hapa Mkoani kwetu kuna mahotel mengi tu na sheli za mafuta nyingi, lakini huwa hawatumii mashine za EFD kutoa risiti wao wanaandika kwa mkono hii haikubaliki ni sawa na luhujumu uchumi wa nchi"alisema Msanjille.

Pia umoja huo umempongeza mwenyekiti wa wazazi Taifa Alhaji Bulembokwa kuadhimisha wiki ya wazazi katika jumuiya hiyo ambapo Kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mimi binafsi ni raia wa kawaida na ninaunga mkono hoja kama hii ya kuhakikisha maendeleo ya Mkoa wetu waKigoma wenye raslimali nyingi na zisizo bado kutumiwa, na maendeleo ya Taifa kwa ujumla wake. "Vijana msilale bado mapambano" wahenga walinena. Daima mbele

    ReplyDelete
  2. Hakika nakushukuru ndugu kwa kuinga mkono. Ikumbukwe kuwa maendeleo hayana vyama wala dini. Tunachotaka ni resources tulizonazo zitufae katika ustawi wa MKOA wetu na Taifa kwa ujumla. Vijana tuungane kwa mawazo chanya ya maendeleo ya Kigoma

    ReplyDelete
  3. Ajabu ni kwamba vyama vingine vya siasa vinangoja siku ya kushika dola ndipo vionyeshe au vijiunge katika kuikomboa Tanzania yetu na wakati huo huo vinalia eti tuachane na mishikamano ya kivyama kwa ajili ya maslahi ya taifa! Huu ni unafiki mtupu!

    ReplyDelete
  4. Hakika! Tunapaswa kuibadili jamii yetu sisi wenyewe

    ReplyDelete
  5. Lakini pia tushiriki kumuunga mkono mkuu wa Nchi kwa jitihada zake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...