Waandishi wa habari
wameaswa kujiendeleza kielimu katika fani ya uandishi wa habari na taaluma
nyingine ili waweze kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
jamii.
Wito huo umetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria Dr. Hamza Kondo alipokuwa
akizindua kitabu chake kiitwacho Watchdog Journalism in Tanzania a Sustainable
Struggle ambapo kwa Kiswahili ni “Uandishi Habari Huru Tanzania ni mapambano
endelevu”.
Dr Kondo amesema
lengo la kitabu hicho ni kuwaelimisha na kuwaasa waandishi wa habari na
wataaluma ya habari kuzidi kuithamini taaluma hiyo licha ya changamoto
zinazowakabili.Amesema kitabu hicho
kinazungumzia uhalisia wa uhuru wa habari nchini, hivyo kinafaa kufundishia
taaluma ya habari katika vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini.
Aidha, Mhadhiri huyo
ameongeza kuwa ili fani ya taaluma ya habari iheshimike ni lazima iwe na bodi
ya wataalamu waliobobea ambayo itaundwa na wasomi wa taaluma husika ili
kusimamia maadili ya taaluma hiyo na kuchukua hatua kwa wanataaluma
watakaokiuka maadili.
Mbali na hayo Dr
Kondo ametoa zawadi ya vitabu kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini likiwemo
gazeti la Jamuhuri, gazeti la majira, gazeti la Habari Leo, gazeti la Mwananchi
na gazeti la Nipashe.
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...