Mgogoro uliokuwa unaashiria kuvunja amani kati ya vijiji viwili Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),ulitulizwa na wakuu wa wilaya ya Kilolo Mh Selemani Mzee na  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ambao walipofika kwenye eneo la tukio na kukutana na wananchi wa vijiji vyote viwili ambao walikuwa na hasira huku kila mmoja akidai mwenzie kaingilia eneo la mwenzake. 

Katika mgogoro huo eneo la kijiji cha kitongoji cha Igominyi kwenye gazeti la serikali linaonyesha kipo Kijiji cha Ilore (Kilolo) lakini kwenye ramani ya mpaka wa wilaya kinaonyesha kipo Ilambilore (Iringa). wakuu hao waliahidi ndani ya siku 30 wataleta jibu.

Mkuu wa wilaya ya Kilolo alipiga marufuku wananchi kujichukulia madaraka na kuanza kufyeka msitu. Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Kasesela aliagiza wafugaji wasivushe kabisa mifugo yao kwenda upande wa wenzao. Pia ni wakati mufaka wafuigaji wakaacha kuwa wachungaji bali wafugaji hii iwe ni pamoja na kubadili aina ya mifugo.

Mfugaji maarufu aitwaye Selemani alilaumiwa kwa mifugo yake kuvuka na kula mazao katika mashamba ya watu. Mkuu wa wilaya ya Iringa alimuamuru Mfugaji huyo kulipa kiasi cha shilingi 90,000/ na debe 2 za mahindi. Pia kufanya tathmini ya shamba la mkulima mwingine ili nalo lilipwe fidia. kikao hicho kiliisha mnamo majira ya saa 10 jioni.
Kikao hicho kikiendelea  kati ya wananchi wa kijiji cha  Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),kufuati mgogoro wao wa mipaka kati ya kijiji na kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela  akizungumza na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela  akipewa ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi nyumba kwenye picha ya kwanza katika miaka michache ijayo zibaki kwenye vitabu vya historia. Tukinuia na kuhamasishana tunaweza kuboresha makazi na hali ya wananchi wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...