Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro amesema kuwa gari hilo sio mali ya Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam, bali ni moja ya gari linalomilikiwa na watu binafsi ambao wanasaidiana na Dawasco katika kusambaza huduma ya maji maeneo ambayo huduma hiyo bado haijafika kwa kutumia magari makubwa ya kusambaza Maji (maboza) ambayo yamesajiliwa na kuwekwa nembo ya Dawasco.

“Gari hili sio mali ya Dawasco, bali limesajiliwa na Dawasco na kuwekewa viambatanisho vyote muhimu ili kusambaza huduma ya Maji maeneo ambayo mtandao wa Maji haujafika haujafika” alisema Lyaro.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Dawasco ilianza zoezi maalum la kusajili visima pamoja na magari yote makubwa ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es salaam, ambapo tayari magari makubwa takribani 256 ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es Salaam yamekwisha sajiliwa.

Dawasco inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia taratibu za kazi kwa kuandika taarifa zenye uhakika na ukweli ili kuepuka upotoshaji wa habari kwa wananchi.

Everlasting Lyaro 
Kaimu Meneja uhusiano- Dawasco
022-2194800 au 08001164
Dawasco Makao Makuu

30/05/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...