Na Bashir Yakub.
Mara kadhaa imetokea mtu anahitaji kununua ardhi sehemu ambayo yeye haishi. Mara nyingi hii imetokea kwa walio nje ya nchi. Mtu anaona kiwanja au nyumba kwenye mtandao au kwenye chombo chochote cha habari lakini anakosa namna ya kununua.
Saa nyingine hufanya mawasiliano na wahusika hadi kufika bei lakini tatizo likawa ni vipi atanunua. Vipi ataweza kununua bila kuhitaji kurudi nchini hubaki mtihani.
Anapiga mahesabu ya nauli kwenda na kurudi, usumbufu, ratiba ya kazi zake na mambo mengi anaona haiwezekani. Anashindwa kununua kwasababu tu ya umbali. Na hii si kwa walio nje ya nchi tu bali hata walio mikoa tofauti pia hili huwatokea japo si sana.
Pia wako wengine ambao tatizo sio kuwa mbali na maeneo wanayotaka kununua bali wana shughuli nyingi mno kiasi cha kutopata mda mzuri wa kufuatilia miamala ya manunuzi mpaka mwisho.
Hawa wote na wengine wengi kupitia makala haya watajua namna ambavyo wanaweza kununua ardhi bila kuhitajika kuwepo.
1.TARATIBU ZA KUNUNUA ARDHI.
Imewahi kuelezwa mara nyingi namna bora na salama ya kununua ardhi lengo likiwa hasa kuepuka utapeli, kuepuka kuuziwa mara mbili au zaidi kwa watu tofauti( double allocation), kuepuka kununua maeneo yenye migogoro mahakamani, maeneo yaliyowekewa mazuio( injuction & caveat), kuepuka kununua maeneo yasiyo na hati za mirathi, yaliyowekwa dhamana n.k.
Tulieleza hatua za kufuata ili kuyaepuka haya sambamba na maandalizi ya mkataba wa mauzo yanayokidhi vigezo mahususi vya kisheria. Ni vema kila mda kusisitiza kuwa migogoro ya ardhi inazidi kuongezeka kila siku na watu hupata hasara kila kukicha. Lakini unaweza kuepuka kuwa sehemu ya migogoro hii ikiwa tu utafuata taratibu pamoja na kuzingatia maandalizi mazuri ya mkataba wa mauzo unaokidhi vigezo vya kisheria.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Ila sitofanya hivyo kwani atanikata pesa.
ReplyDelete