Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Wa Pili kulia) akiwa na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita, waliohudhuria kikao baina ya Waziri na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Kikao kililenga katika kujadili suala la magwangala na maeneo ya wachimbaji wadogo nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...