JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.
Katika
Tukio la Kwanza:
Mtoto wa miaka mitatu
aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN
mkazi wa Matemela Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo
baada ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu Journey ikiendeshwa na dereva aliyefahamika
kwa jina la ELIABU MYEKO (33) mkazi
wa Makambako Mkoa wa Njombe.
Tukio hilo limetokea
mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko katika Kijiji cha
Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo. Dereva alikimbia mara
baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na mmiliki wa Gari
zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhi Kituo cha Afya Ipwani Wilayani
Mbarali kwa uchunguzi wa kitabibu.
Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL
G. LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto
ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani
ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye
taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu azitoe kwa mamlaka husika
ili akamatwe.
Katika
Misako:
Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na
miche 25 ya Bhangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.
Mtuhumiwa alikamatwa
katika msako uliofanyika mnamo tarehe
01.02.2016 majira ya saa 16:00 jioni
katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya
Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha
katika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19) mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram 10.
Mtuhumiwa alikamatwa na
askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe
01.05.2016 majira ya saa 17:05 jioni
huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya
Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa watafikishwa
mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.
Imesainiwa na:
(EMANUEL G.
LUKULA – ACP)
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
Idara nyeti ya umma, kama Idara ya Polisi, kutumia anwani ya baruapepe ya bure, kama hiyo ya gmail.com ni skandali kubwa. Anwani hiyo inadhalilisha heshima na utu wa Idara ya Polisi. Kwa nini iwe ya bure; hivi pesa hawapewi au zinazalisha majipu?
ReplyDelete