001Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua rasmi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam ambapo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ambayo wafanyakazi wake wanaifanya kwani ndiyo shirika pekee la Serikali linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na kuiletea heshima serikali, Waziri Mabula amewaambia wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na Menejimenti yake kuendelea na kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ili kuleta maendeleo zaidi nchini katika sekta ya nyumba.
PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE.
11 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2016

    Unawasifia nini, hawa jamaa ni bure kabisa. Nyumba za Mwongozo zilikuwa ziishe Machi 2015, sasa hivi hata wenyewe hawajui zitaisha lini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2016

    Hongera Rais Magufuli kwani vinginevo mikutano yote hii ingekuwa nje ya dar kwenye mahoteli ya star saba kumbe kumbi za maana kabisa zipo mjini. Shukrani NHC kwa kuonyesha mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2016

    Hongereni!Kazi nzuri na nyumba ni nzuri sana. Ila mikopo imewekewa riba kubwa sana ambayo huwezi kumaliza deni kirahisi. Nyumba ni asset isiyo hamishika na mkopo wake ni wa miaka mingi,hivyo kuweka riba ya 8% kwa miaka 15 ni wizi wa hali ya juu kutoka kwa mabenki yetu.
    Maana kwa mfano ukikopa milioni 200 (200,000,000) riba peke yake kwa mwaka wa kwanza ni 16,000,000(16 million) ;ambayo ni karibu na 1,300,000 kwa mwezi. Hii ni riba tu ,bado hujaweka malipo ya yanayoingia kwenye mkopo wenyewe labda 1,000,000, jumla inakuja kama 2,300,000 kwa mwezi.

    Hii itasababisha anguko la kiuchumi kwenye hiyo sekta ya real estate.
    Kama ilivyotokea USA, mabenki mengi yatafilisika kwa sababu wengi watashindwa kulipa hayo madeni.

    Ni mamoni yangu tu...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2016

    NHC anzeni kujenga majengo kwa kutumia wafanyakazi wenu. Tabia ya kuwapa wakandarasi binafsi na wa kutoka nje itumike kama chachu ya ninyi kujifunza. Wakati umefika muweze kujitegemea wenyewe kwa kutumia resources zenu ili kuokoa pesa mnazolipa wakandarasi wengine.
    Hii italeta tija kwa wakandarasi wenu pia bei za nyumba zitakuwa nafuu kwa watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...