WAKAZI wa Kijiji la Mnavila, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, wamefanikiwa kuwaua Mamba wawili waliokuwa wakisumbua kijijini hapo kwa matukio ya kudhuru watu kwa kuwajeruhi na wengine kuuwawa kwa kuliwa na Mamba hao.
Wananchi hao ambao makazi yao yapo kando kando ya Mto Ruvuma, wamekuwa wakipatwa na majanga hayo kwa kipindi kirefu, hali iliyowapelekea kuomba msaada kwa Kampuni ya OnTour Tanzania yenye makazi yake jijini Dar es salaam ambayo ina kibali cha kuwinda Mamba wahalibifu hasa katika mikoa ya Ruvuma na
Mtwara.
Mamba hao wamekuwa ni tishio
sana kwa binadamu, hasa wale wanaotumia Mto huo kwa matimizi mbalimbali, na kupelekea watu wengi kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamepoteza
viungo na kuwafanya wawe na vilema vya kudumu.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mnavila, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakishirikiana na Maafisa wa Kampuni ya OnTour Tanzania, kumshusha mmoka wa Mamba hao, baada ya kuwaua kutoka na madhara ya kuwadhuru wakazi wa kijiji hicho.
Sehemu ya Wanakijiji hao wakiwa wamewazunguka Mamba hao baada ya kuwaua ili waweze kutoa miili ya watu walioliwa.
Mtaalamu wa kuwapasua Mamba hao, akiendelea na kazi yake ikiwa ni jitihada za kuutoa mwili wa mmoja wa Wanakijiji hao alieliwa na Mamba hao hivi karibuni.
TATIZO KUBWA SANA SERIKALI YA TANZANIA INAONA WANYAMA NI BORA KULIKO RAIA WAKE.TUMEPIGA KELELE SANA MAMBA WAMEONGEZEKA SANA MTO RUVUMA,ZIWA RUKWA MTO MALAGALASI NA ZIWA VICTORIA LAKINI HAKUNA HATUA ZINAZOCHUKULIWA.ONA MPAKA MAMBA ANAUWAWA NA TUMBONI ANATOLEWA BINADAMU HII NI AIBU KWA NCHI HII ISIVYOJALI RAIA WAKE."SASA KAZI" IPO KUTUMBUA WATU TU LAKINI SI KUJALI UHAI WA RAIA WAKE.MALIZENI TATIZO HILI NI AIBU WAZIRI NA WATU WAKE WA MALI YA ASILI HAIJULIKANI HAIJULIKANI WANAFANYA NINI MPAKA WANANCHI WANAPIGA KELELE LAKINI HAWASIKILIZWI,IPO SIKU WANANCHI WATAWAUWA KWA SUMU HAWA WANYAMA,KWANI WANANCHI WAMECHOKA.
ReplyDeleteMamba waliumbwa na kupewa mazingira yao. Ukiyaingilia Kama ambavyo tunazidi kufanya hayo ndio matokeo yake. Ufumbuzi wa tatizo sio kuwaua mamba bali kuheshimu mipaka ya mazingira ya kila kiumbe. Mbona husrmi binafamu tumezaliana sana na kuingilia mapori na maeneo ya wanyama pori? Lazima tujue jinsi ya kuishi na viumbe hivi. Hata sisi tuheshimu mpango wa uzaxi. Anayelalamika si ajabu ana watoto kumi! Ni rahisi kuilaumu Serikali kila kitu hata uzaxi wake mwenyewe bake athari zake. Please.
ReplyDelete