Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani akiwaelimisha wanafunzi wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyoko mkoani Geita kuhusiana na Mfuko wa Penseheni wa PSPF na lengo la kusaidia jamii katika hususan katika masuala ya elimu. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni hapo.
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani) pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2016

    jamani achana na kuwapa watoto mabegi zisaidieni shule ziwe na program walau watoto wapate chai mashuleni,huko vijijini kuna watoto wanaenda shule bila hata kunywa chai maana familia haina uwezo.mtoto hawezi kuelewa darasani akiwa na njaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...