Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen Kahatano akizungumza na waahabari juu ya nauli za mabasi yaendayo kasi haraka katikati ya jiji la Dar es Salaam,kutoka Mbezi mwisho –Kimara –Kivukoni nauli ni800 mwanafunzi 200. Mbezi mwisho –Kimara –Kariakoo nauli 800,mwanafunzi200. Morocco-Kimara –Mbezi Mwisho nauli 800,mwanafunzi 200. na Morocco-Kivukoni nauli 650. mwanafunzi 200. Kariakoo – Morocco nauli 650.mwanafunzi 200.viwango vipya vya nauli vinapaswa kuanza kutumika rasmi Mei,12 mwaka huu, mkutano huo umefafanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Traffic wa Kanda, Magembe Seni.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen Kahatano leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii.
Je kuna uwezekano wa wasafiri wa mabasi hayo ya kasi kununua ''tiketi'' ya msimu kwa kulipa ''in-advace'' kwa mwezi mzima akapanda mabasi hayo ya route zote kwa mwezi mzima kwa kuonesha kadi ya malipo aliyolipia yaa mwezi mzima in-advance na hivyo kupunguza kulipia kila siku kwa kila route.
ReplyDeleteUtaratibu wa kulipia tiketi in advance kama wa voucher za simu/umeme pia kuwezesha kampuni ya mabasi ya mwendo kasi kupata malipo in-advance kununulia mafuta, vipuri pia kuingia maktaba na makapuni ya mafuta/matairi/vipuri/ununuzi au ku-''hire'' mabasi ya ziada kwa pesa hizo za ''advance''
Nakumbuka kampuni ya Usafirishaji ya Dsm a.k.a UDA Enzi za Mwl. Nyerere walikuwa na utaratibu huo wa kulipa ina Advance na pia nikaukuta nchi nyingi za ulaya wanafanya utaratibu huo na ukiwepo usimamizi mzuri basi hakuna shaka route za mabasi ya mwendo kasi DSM utapanuka mpaka Wazo Hill, Mbagala n.k
Ndivyo inavyotakiwa iwe. Shida tunataka vitu vya gharama lakini uwezo wa kuvihudumia ni mdogo.
ReplyDelete