Aprili 29, 2016 Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya Heshima jijini Toronto, Canada. Mkataba huo ulitiwa saini kati ya Konseli wa Heshima, Bw. Deepak Ruparell na Mhe. Jack Mugendi Zoka Balozi wa Tanzania Nchini Canada ambaye aliiwakilisha Serikali ya Tanzania. Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Ottawa nchini Canada

Tukio la kutiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya Heshima jijini Toronto, Canada likifanyika kati ya Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Tanzania nchini Canada ambaye anaiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell , likishuhudiwa na maafisa wa Ubalozi.
Baada ya tukio la kutiliana saini mkataba, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka na Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell , wanaonekana wakibadilishana nyaraka za tukio hilo.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell nakala ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1963 kuhusu Utendaji wa Shughuli za Kidiplomasia na Taratibu za Kikonseli ikiwa ni moja ya vitendea kazi muhimu kwa matumizi ya ofisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...