Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAMILIKI wa  Daladala wamelalamikia utaratibu wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwa kuondoa daladala katika barabara ya Morogoro ambayo ni kinyume na makubaliano.

Akizungumza na waandishi jiji Dar es Salaam, Mmiliki wa Daladala , Kassimu Kimaro amesema kuwa daladala zimeondolewa zitafanya kazi wapi na hakuna maelezo ya kutosha juu kuondolewa kwa daladala hizo.

Amesema kuwa kwa mujibu wa mkataba walitapewa milioni nne ikiwa milioni moja kwa ajili ya hisa katika UDART lakini maamuzi hayo waliyapinga na baadae wakaona fedha hizo katika akaunti na hazina maelezo.

Kassimu amesema kuwa kutokana na mradi huo wanachotaka daladala zao wazinunue UDART ili waweze nao kuendesha biashara nyingine nje ya Daladala.

Amesema kuwa hawezi kukubali kuweka daladala zao nyumbani wakati ndio biashara zao katika kuendeesha maisha na hawana kitu kingine cha ziada.

Aidha amesema katika utaratibu huo wameumiza watu wengi ambao wanategemea dalaladala pamoja na madereva  kukosa kazi kuendesha daladala hizo.
Ameiomba serikali kuangalia upya juu ya wamiliki wa daladala ambao hawako katika uendeshaji wa udart huku wakiwa na hisa ambazo hawajui faida zake na fedha wakiwa wamekata katika hisa hizo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...