Na: Lilian Lundo – Maelezo
Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa kutuma maombi yao shirika la “Master Card Foundation, Fund For Rural Prosperity” ili kupanua na kuimarisha upatikanaji wa fedha Vijijini Tanzania.
Hayo yalisemwa na Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti leo, jijini Dar es Salaam katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.
Aidha, Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Jumla ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaoishi maeneo ya Vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020.
Mtaalam
Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa
waandishi wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato
lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa
kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo
ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa
kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Mtaalam
Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akifafanua jambo
katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya
kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada
wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo
Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...