WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KULAANI MAUAJI YA WATU SABA (7) WA FAMILIA MOJA WILAYANI SENGEREMA MKOA WA MWANZA

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na tukio la mauaji ya watu saba wa familia moja waliokatwakatwa mapanga baada ya kuvamiwa nyumbani, katika kijiji cha Sima wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, siku ya Jumatano usiku. 

Wizara inalaani vikali mazingira ya mauaji ya watu hao wa familia moja, ambapo wauaji walivamia nyumba ya mama mjane na kumuuwa yeye mwenyewe, na watu wengine sita wakiwemo watoto watatu.   

Wizara inapongeza utayari wa uongozi wa mkoa wa Mwanza na jeshi la Polisi amabo waliweza kufika sehemu ya tukio ili kufuatilia mauaji hayo. Ni imani ya Wizara kuwa Polisi kwa ushirikiano wa wananchi wa wilaya ya Sengerama wataweza kuwasaka watuhumiwa wa mauaji na  kuwachukulia hatua kali.   

Wizara inawasisitiza wananchi kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwamata watuhumiwa ili kuondoa hofu miongoni mwa familia za kijiji cha Sima na wilaya ya Sengerema. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kutarejesha imani na utulivu miongoni mwa wakazi wa Sengerema na hivyo kuweza kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
 
Wizara inasisitiza kwamba  kila binadamu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya mauaji ya kikatili vinapotokea katika familia zetu vinasababisha hofu kubwa miongoni mwa wanafamilia. Mauaji hayo yanawakosesha amani wanafamilia na yanadhohofisha ari ya ndugu wa familia kufanya shughuli zao kwa amani.   

Wizara inaomba wanafamilia waliopoteza ndugu zao kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa, wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo.

   Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
                      Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.  12/5/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2016

    Poleni wafiwa. Kila mtu athamini uhai mauaji ya kiholela yasipate nafasi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...