Yale
mabasi yaendayo haraka, tuliyokuwa tukiyasubiri kwa hamu kwa kipindi
kirefu, hatimae leo yameanza kazi rasmi kwa ruti zote zilizopangiwa.
pamoja na kuanza kwa kazi, lakini bado wanachangamoto ya matumizi ya
njia yake, kwani bado kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vimekuwa
vikiitumia njia yake hiyo kana kwamba ni jambo la kawaida tu. Leo Kamera
ya Mtaa kwa Mtaa imezungukia eneo la Kariakoo na kujioneka hali halisi
katika barabara hiyo na kukuletea wewe mdau ujionee mwenyewe na kutoa
maoni yako ya nini kifanyike ili jambo hili likae kwenye mstari
ulionyooka. Picha na Emmanuel Massaka.
Daladala
hili likiwa limeifunga kabisa njia hiyo kwa lengo la kukatisha barabara
hiyo kurudi lilikotoka baada ya kuona chombo chenye njia yake
kikichomoza mbele yake.

Bodaboda na Watembea kwa miguu wakijidai katika barabara hiyo.
Ssa hawa watembea kwa miguu kwa nini wanatembea katika kati ya barabara, na Bodabodaje?
ReplyDeleteLazima ifikia mahali watanzania waache ujinga na ukorofi kwa kigezo cha ugumu wa maisha. Ndio maana Rais anakuwa mkali watu wanaanza oh sijui nini. Hawa wote ilibidi wachukuliwe sheria. Lazima watu wafuate sheria.
ReplyDeleteInabidi ziwekwe kamera hapo watakao pigwa picha walipe fine kubwa na dereva kunyang'anywa leseni ....au serikali iweke fence
ReplyDelete