Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda  (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda 2015 (PMAYA) iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi wetu
Nia serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuanza kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa nchini ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kusaidia kuinua uchumi wa nchi lakini pia kutoa ajira kwa watanzania katika viwanda vinavyoilikiwa na matajiri hao.
Hilo limenza kuonekana siku moja baada ya Rais Magufuli kuweka wazi nia yake hiyo ambapo Mo Blog ilifanikiwa kupata picha ambayo ilimwonesha Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza mambo mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Taznzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi mara baada ya kumalizika kwa halfa ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda (PMAYA) zilizoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Kutokana na muonekano wa viongozi hao wawili wa serikali na sekta binafsi ni wazi kuwa serikali ya Rais Magufuli imejipanga kushirikiana na wafanyabiashara ili kufanya kazi kwa pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda jambo ambalo litachangia ukuaji wa kasi wa uchumi na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2016

    Wafanya biashara wakubwa pia wanaweza kuwa na code of conduct kupitia vyama vyao kuhakikisha kwamba wanachama wao wanafanya biashara halali kufuatana na taratibu zilizopo na sheria. Mkakati na mipango ya kupanua kundi hili na kuwezesha wengi ni muhinu pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...