Habari na Picha Na Gabriel Kilamlya
WANGING'OMBE-Njombe
Serikali Wilayani Waging'ombe imesema haiko tayari kuona Shule Inakosa Madawati Hadi Ifikapo Juni 29 Mwaka Huu, Siku Moja Kabla ya Tarehe Iliyotangazwa na Serikali Kukamilika Kwa Madawati Kwa Nchi Nzima.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya Ya Wanging'ombe Dkt. Asumpta Mshama Leo Wakati Akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo.
Hatua Hiyo Ameitoa Wakati Baadhi ya Maafisa Watendaji wa Kata Wakitoa Taarifa Kuwa Wanaupungufu wa Madawati Kitu Ambacho Amesema Hawezi Kuwavumilia Ilihali Agizo Hilo Ni la Muda Mrefu Sasa.
Amesema Kabla Yeye Hajawajibishwa Juni 30 Mwaka Huu Basi Ataanza na Maafisa Watendaji Hao Ambao Wataonekana Kushindwa Kukabiliana na Suala Hilo na Kwamba Hawezi Kuwajibishwa Pekee Yake.
Kwa Upande Wake Afisa Elimu Msingi Katika Halmashauri Hiyo Mwalimu Haruna Mlilapi Amesema Kwa Wastani Halmashauri Hiyo Haina Upungufu wa Madawati Kwani Kuna Zidio la Madawati Licha ya Shule Chache Kuonekana Kupungukiwa Baadhi ya Madawati Ambayo Ifikapo Juni 29 Mwaka Huu Yatakuwa Yamekamilika.
Katika Kata ya Mdandu Mmoja wa Wenyeviti wa Vitongoji Damian Kihombo Toka Ngelele Kijiji Cha Mdandu Pamoja na Fundi Aliyekuwa Akitengeneza Madawati ya Shule Bwana Zacharia Mng'ong'o Wametajwa Kuuza Madawati Hayo na Kutafuna Fedha Jambo Ambalo Afisa Mtendaji wa Kata Hiyo Bwana Timoth Fute Amelazimika Kuwasweka Lumande.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alisema kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya Watakaoshindwa kuchonga madawati na kuonesha upungufu wa madawati katika shule za Wilaya na mikoa yao Hawatamfaa katika Serikali Yake Jambo Lililowafanya Wakuu wa Wilaya Kuumiza Vichwa Kabla ya Kutumbuliwa.
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Dkt. Asumpta Mshama Asema Atawatanguliza Maofisa Watendaji watakaoshindwa kukamilisha utengenezaji madawati ndipo yeye afuate
Mkuu wa Wilaya Ya Wanging'ombe Dkt. Asumpta Mshama Akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo.Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo
Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo
Maafisa Watendaji wa Kata Zote na Wakuu wa Shule Mbalimbali Ambao Wamekutana Kujadili Tathmini ya Utengenezaji wa Madawati Katika Wilaya Hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...