Na Mwandishi Maalum, New York
Imeelezwa kwamba , upatikanaji wa vifaa saidizi  ( assistive divices) kwa watu wenye  ulemavu wa aina mbalimbali   siyo tu,  utawawezesha  kushiriki katika  shughuli  za  kiuchumi, kijamii na maendeleo bali pia utawaondolea  hisia za kunyanyapaliwa na  kubaguliwa.
Hayo  yameelezwa na siku ya  jumatano na   Dkt. Abdallah Possi ( Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri, wakati alipokuwa akichangia  majadiliano  kuhusu  mada ya  uondoaji wa umaskini  na kukosekana kwa usawa    kwa watu wote wenye ulemavu. Mhe Possi alikuwa mmoja wa  wanajopo  watano, walioongoza  majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya pili ya mkutano wa tisa  wa Mkataba wa Watu Wenye Ulemavu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katika mchango wake,  Naibu Waziri amesisitiza kwamba suala la    upatikanajji wa vifaa saidizi  kwa watu wenye ulemavu ni muhimu sana  kwa kile alichosema  ukosefu wa vifaa  hivyo  ni  moja wa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu.
Akatoa wito  kwa  serikali, jumuiya ya kimataifa na asasi   za kiraia  kuangalia ni kwa namna gani katika wa umoja wao  wanaweza kushirikiana ili kukabili changamoto hiyo ya upatikanaji wa  vifaa saidizi wa watu wenye ulamavu.
Mhe Possi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu, pamoja na kuzungumza  uhaba wa vifaa saidizi pia amezungumzia kwa uzito wa aina yake kuhusu pamoja na mambo megine fursa ya upatikanaji wa ajira  kwa watu wenye  ulemavu, unyanyapaji na mitizamo  hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.
 Akasema      mitizamo  hasi  dhidi ya watu wenye  ulemavu, ubaguzi na uyanyapaji  umekuwa  kikwazo kikubwa katika    siyo tu, utekelezaji wa sera na mipango ikiwamo ya  fursa za ajira kwa walemavu, bali pia katika kufungua  fikra na  mitizamo  mipana  na jumuishi kuhusu watu wenye ulemavu.
Aidha  Mhe. Naibu  Waziri amerejea kauli yake kwamba  inakuwa vigumu kutenganisha  ulemavu na umaskini kwa kile anachosema vinakwenda pamoja.
Akasisitiza ili watu wenye ulemavu waweze kushiriki katika utekelezaji wa Agenda 2030, kujipatia fursa za ajira kama  ilivyo kwa watu wengine pamoja na  kuondokana na umaskini, jamii inao wajibu  mkubwa wa kutoa ushirikiano  kuacha kuwabagua, kutowanyanyapa  na kubwa zaidi   kwa watendaji na wenye mamlaka serikali kuandaa na kutekeleza  mipango ambayo ni  jumuishi  na yenye kuzigatia maslahi , mahitaji  na  mazingira halisi ya watu wenye ulemavu.
Hoja ya  vifaa saidizi kwa watu wenye  ulemavu  iliungwa mkono na wanajopo wengine  kwa kile walichoeleza kwamba ni muhimu sana katika  kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa huru na kuondokana na utegemezi.
Wanajopo hao mbali ya  Dkt. Possi  walikuwa ni  Bi. Asa Regner, Waziri  wa   Waziri wa Watoto,  Wazee na Usawa wa Jinsia  kutoka Sweden,  Bw. Joelson Dias ambaye ni  Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati ya  Haki za watu wenye ulemavu kuotka Brazil,  Bi, Silvia Quam kutoka Guatemala na  Bi Emi Aizawa, kutoka Japan.
 Mhe. Dkt. Abdallah Possi, (Mb) Naibu Waziri, Ofisi  ya Waziri Mkuu akichangia  majadiliano kuhusu  mada ya  kuwaondololea umaskini na   kukosekana kwa usawa kwa  watu wenye ulemavu. Mhe. Possi alikuwa mmoja wa wanajopo watano walioanzisha majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya pili ya  Mkutano  wa Tisa wa Mkataba wa Watu  wenye Ulemavu unaoendelea hapa  Umoja wa Mataifa.
 sehemu ya  washiriki  wa  majadiliano kuhusu kuwaondolea umaskini na kukosekana kwa usawa  kwa watu wenye  ulemavu ikiwa ni sehemu ya  mwendelezo wa  majadiliano kuhusu  ajenda kuu ya mkutano wa tisa wa mkataba wa watu wenye ulemavu. 
 Ujumbe wa Tanzania ambao umeongoza na  Mhe, Naibu  Waziri katika  mkutano wa Tisa  wa  Mkataba kuhusu Watu wenye  Ulemavu. 
 Naibu Waziri Possi  akibadilishana   mawazo na   Bi. Asa Regner Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Jinsia  kutoka Sweden muda mfupi  kabla ya kuanza kwa majadiliano kuhusu kuwaondolea umaskini na kukosekana kwa usawa kwa watu wenye ulemavu.
Ujumbe wa Tanzania ambao umeongoza na  Mhe, Naibu  Waziri katika  mkutano wa Tisa  wa  Mkataba kuhusu Watu wenye  Ulemavu.  kati ya wajumbe  hao ni,   kutoka kushoto mstari wa nyuma ni  Bi. Ngusekela Karen Nyerere ( Mambo ya Nje) Mhe. Stella Ikupa Alec ( Mb, CCM), Mhe. Riziki Said Lulinda( Mb,CUF) na Mhe. Dkt. Elly Marko Macha( Mb. CHADEMA)  aliyekaa mbele ni  Bi Josephine Makunzo Lyengi, Kaimu Kamishna kuhusu Watu wenye Ulemavu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...