Baada ya Kikosi cha timu ya EFM REDIO kuwatandika Timu ya Bongo Fleva magoli 4 kwa 3 sasa inajifua kwa ajili ya mpambano wake na Timu ya SINGELI FC katika mechi itakayochezwa siku ya jumapili, tarehe 03/07/2016 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, Jijini Dar es Salaam. 

Mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10:00 Jioni hadi saa 12:00 Jioni itavikutanisha vikosi vikali vya Timu mbili ambapo kikosi cha Efm Redio kitaongozwa na wachezaji mahiri akiwemo Maulid Kitenge, Dennis Ssebo, Omary Katanga, Rdj Manzi,Mohamed Lukwilu, Juma Mtoro na Ibrahim Masoud (Maestro), na kikosi cha wanamuziki wa Singeli kitaongozwa na Sholo Mwamba, MCzoo, Majid Migoma, Maseke na wengineo Mechi hiyo baina ya wafanyakazi wa kituo cha redio cha efm na wasaani wa muziki wa singeli kina Lengo la kufahamiana na kudumisha urafiki uliopo kati ya EFM redio na wasanii wa singeli nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...