Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Hawa Ng’humbi akizungumza na baadhi ya wataalam wa masuala ya maafa walipomtembelea ofisini kwake ili kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Juni 16, 2016.
Mnufaika wa mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa Bi. Juliana Peter akifurahia mbuzi wa mradi huo wakati wa zoezi la Tathimini ya utekelezaji wa mradi huo lililofanywa na Wadau wa masuala ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 16, 2016.
Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa katika Maeneo yaliyoathirika na Ukame Bw.Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akifuatilia mtoa mada (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kujadili utekelezaji wa mradi huo, Wilaya ya Kishapu tarehe 16 Juni, 2016.
Baadhi ya wanakikundi cha Muungano wakifurahia mafanikio ya kuongezeka kwa mbuzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa wakati wa tathimini ya utekelezaji wake iliyofanywa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri mkuu tarehe 16 Juni, 2016 Wilaya ya Kishapu Shinyanga.
Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Mazingira Bi. Juliana Peter akichangia hoja wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kujiandaa na Kupunguza Athari za Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 16, 2016.
Ushirikishwaji wa walengwa katika mipango na miradi yote ni muhimu kama tunataka mipango inaayolenga wananchi ifanikiwe.
ReplyDelete