Uendeshaji wa magari wa aina hii unaleta kero na adha kubwa kwa madereva wengine barabarani,Uendeshaji huu wa kutofuata sheria za usalama barabarani,Jeshi la Polisi liongeze kasi kupambana na kuwadhibiti vilivyo madereva wa aina hii,ambao kwa makusudi mazima huamua kukiuka sheria hizo na kupelekea usumbufu mkubwa kwa madereva wengine wenye kutii sheria.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga ameeleza leo kuwa ongezeko la makosa ya watumiaji wa barabara limechangia jeshi hilo kuagiza askari wake kukamata watumiaji kumi kila siku wanaovunja sheria za barabarani.

Kamanda Mpinga alibainisha Makosa yanayofanywa na madereva wengi ni pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking),(tazama picha juu na chini), kupita taa nyekundu, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha wakiwa wamelewa, madereva bodaboda kutovaa kofia ngumu, kubeba mishikaki, kutokuwa na leseni na pikipiki kutokuwa na Bima.

Na sisi Globu ya Jamii katika kuliunga mkono Jeshi la Polisi,Kikosi cha usalama barabarani,liendelee kukaza uzi kukamata makosa kumi kila siku ya madereva wazembe barabarani mpaka tunyooke. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2016

    Hili jambo Jeshi la polisi limeshindwa kusimamia kwa juhudi thabiti uendeshaji mbovu. Madereva wanapata (wanajenga) kiburi kwa vile sharia imelifumbia macho hili jambo. Wazee wa favor mmepewa target ya magari kumi kwa siku.. Kazi kwenu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...