Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na biashara ya maji ya kwenye vifuko maarufu kama viroba ambayo pia yana jina lingine ambalo ni gumu kidogo kutamkwa hadharani kutokana na matumizi yake, akipanga maji yake hayo kwenye ndoo tayari kwa kuingia nayo mtaani kuyauza kwa wanywaji. Maji hayo ambayo huuzwa kifuko kimoja kwa sh. 50, yamekuwa yakinywewa sana na watu wa kipato cha chini katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, hasa kutokana na wengi wao kushindwa kuhimili gharama za Maji yaliyopitia viwango vyote vya usalama wa afya ya mnywaji. 
 Mdau huyo akijazia maji kwenye kifuko kilichopungua ili kufukia kiwango husika.
 Na huu ndio mtindo wa Maji hayo yanavyojazwa kwenye vifuko hivyo.
Wadau wakikata kiu na maji hayo ya Viroba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2016

    Kila awaye anatambua hatari iliyopo katika maji hayo na walewanayoyatumia hufanya hivyo sababu hawana uwezo wakuyafikia hayo yenye viwango na pia yanapatikana ki rahisi. Mamlaka husika za afya katika jiji la Dar Es Salaam najua wanayaona hayo na hata hao mapolisis na vyombo vingine vya usalam vingefanya ustaarabu kwa kuwaambia hao wanaofanya biashara hiyo wasiifanye kwani inahatarisha afya za wengi. Jamani Mamlaka husika fuatilieni hilo. Si lazima Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aanze kufukuzana na wauza maji ya viroba, yeye anyao majukuma mengi katika mkoa wetu huu hebu tuwe na nyuso za aibu tufuatilie mambo haya.

    Nina amini kikubwa kuwa watu wenye amana za afya mijini kushirikiana na Mamlaka husika katika maeneo na vilevile kushikisha jeshi la Polisi tutafanikiwa kwa hili.

    NAwaomba wahusika kwa heshima na taadhima na tumieni hizo gari na mamlaka mliyopewa kutekeleza hayo.

    ReplyDelete
  2. ipo kazi kumaliza kipindupindu dar


    ni kazi pia kuwa ki0ngozi kwenye Jiji kama hili amabpo unatakiwa uweke dustbirn kweny mbongo za watu wakuelewe vizuri

    milipuko ikija wanalamu viongozi tena wakali wa kutka misaada, mtu anedesha gari kali anakunywa maji anatua chupa ovyo mafuriko a=yakija wanalaumu viogozi

    itafika wakati viongozi wetu watadai bili za panadol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...