TIMU ya Mbeya City imeanza mikakati yake ya kujiandaa kwa msimu mpya huku uongozi wa timu hiyo ukiamua kuingia msituni na kuamua kwenda nchini Malawi kucheza michezo mitatu ya kirafiki.

Kwenye ratiba hiyo, City  imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka ‘dimbani’ Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18  kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo.

Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano  kwenye kikosi cha City, Dismas amesema kuwa mchezo wa pili  nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni  21 na kumalizia na Mzuni Juni 25.

“Baada ya mchezo huo  wa pili jijini Lilongwe,tutarudi kwenye mji  ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 huu utakuwa mchezo wa mwisho kwenye ziara hii ya michezo ya kirafiki, baada ya hapo tutarudi nyumba tayari kwa michezo mingine ambayo  imepangwa ukiwemo  dhidi ya Simba tutakaocheza Morogoro,"amesema Ten. 

Kama mambo yatakwenda sawa, ratiba hii inaweza kuwa na ongezeko la  michezo miwili ya kirafiki katikati ya mwezi julai kabla ya mchezo wa mwisho wa mwezi huo dhidi ya Simba na mwingine  mwanzoni mwa mwezi wa nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...