Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (katikati) akiwa tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, Joyce Shaidi na Kulia kwake ni Mkurugeni Mkuu wa Mfuko huo, Daud Msangi. wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Osward Urassa (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Ahmed Kilima.  Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni "Hifadhi ya Jamii kwa Kila Kaya".
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Daud Msangi, akitoa hotuba yake ya ufunguzi iliyoambatana na taarifa fupi ya Mfuko huo, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya leo Juni 23, 2016.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF),  Joyce Shaidi wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango mpya wa Bodaboda (Bodaboda Scheme), leo Juni 23, 2016 katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa, Jijini Mbeya.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akimpongeza mmoja wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Mbeya ambayo ni wanachama wa Mfuko wa GEPF kwa kuwa wanachama wapya katika Mpango huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...