Bi. Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited na Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena wakishiriki kazi ya kupaka rangi kwenye jengo linalotumiwa na wanafunzi wa kituo cha mafunzo kwa vijana cha Multpurpose Training Center kilichopo Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kulia chakula jana, Kampuni za Montage Limited, Serena Hotel na Benki ya NMB ziliungana kwa pamoja na kukipa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo rangi, madaftari, mafuta ya kupaka chakula vifaa vingine katika kituo hicho vyenye thamani ya shilingi milioni tano.
Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena akipaka rangi kwenye ukuta wa jengo hilo huku wafanyakazi wenzake wakimuangalia.

Mratibu wa kituo cha MTC Bw.Issa Buzohela akielezea jambo wakati ugeni huo ulipotembelea kwenye darasa la vijana wanaojifunza ufundi seremala kituoni hapo.

Hawa ni wanafunzi wanaojifunza kushona nguo kutuoni hapo wakiendelea na mafunzo.

Kituo hiki pia kinatoa mafunzo ya kuzima moto na uokoaji haoa wanafunzi wakiwa tayari wamevalia ngua maalum kwa ajili ya kuokoa mtu aliyenasa kwenye jengo refu linalowaka moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...