Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda (kushoto) akiwasili kwenye Makao Makuu ya NHIF kwa siku ya kwanza mara baada ya kuteuliwa na kuwa mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Raphael Mwamoto pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Eugen Mikongoti. Mh. Makinda alipata, pia fursa ya kuwa na mazungumzo mafupi na uongozi wa Mfuko huo chini ya Kaimu Mkuu wake, Bernard Konga na vilevile alitembelea baadhi ya ofisi ikiwemo kituo cha utunzaji nyaraka za mfuko kwa njia za kielektroniki, kituo cha huduma kwa wateja na kituo cha utunzaji taarifa za Mfuko kwa lengo la kuona jinsi zinavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF), Mama Anne Makinda akiwa katika chumba maalum cha kuhifadhi
nyaraka mbalimbali za wanachama wa mfuko huo leo mara baada ya kufanya
ziara kutembelea Makao Makuu ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akionyeshwa sehemu ya
kuhifadhia kumbukumbu za wanachama mara baada ya kufanya ziara
kutembelea Makao Makuu ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti leo jijini
Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...