NHIF Mkoa wa Morogoro washerekea siku ya Mtoto wa Afrika kwa Kutoa elimu juu ya fao la TOTO AFYA. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Morogoro Bi. Agnes Chaki akitoa maelezo kwa wananchi juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko huo , katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoa wa Morogoro.
Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza wananchi walifika kwenye banda la NHIF Mkoani Morogoro kutoka (kushoto) ni Afisa matekelezo Enock Humba, Agnes Chaki na Hamidu Mwambungu, katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Morogoro.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Agnes Chaki pamoja na Afisa matekelezo wa ofisi hiyo Bw. Enock Humba wakiendelea kuhamasisha wazazi juu ya umuhimu wa Fao la TOTO AFYA, katika siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...